Published On: Wed, Jan 31st, 2018

Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro imeahirisha kesi inayowakabili wabunge wa Chadema.

Share This
Tags

Mahakama ya hakimu mkazi mkoani Morogoro kwa mara nyingine imeahirisha kesi inayowakabili wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  Peter Lijualikali wa jimbo la Kilombero na Suzani Kiwanga wa jimbo la Mlimba na watuhumiwa wengine hamsini na nne, na kwamba kesi hiyo itatajwa tena February 27  mwaka huu kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kutokana na upelelezi kukamilika.

Kesi hiyo namba 296 iliyotajwa  leo mahakamani hapo  mbele ya hakimu mkazi Ivan Msaky, ambapo watuhumiwa 53 walifanikiwa kufika mahakamani hapo huku mtuhumiwa mmoja kutoweza kufika kutokana na kuwa magereza akitumikia kifungo kwa shitaka lingine na kuwakilishwa na  wadhamini wake wawili.

Baada ya Taarifa hiyo ya kutokuwepo kwa mtuhumiwa huyo hakimu Ivan Msaki akawataka wadhamini wa mtuhumiwa huyo kuwasilisha taarifa zake ili mahakama iwasiliane na magereza mkoa wa Morogoro ili mtuhumiwa huyo aweze kuletwa siku ambayo kesi itatajwa tena mahakamani hapo.

Kwa upande wake wakili wa mashitaka Gloria Rwakibarila, ameieleza mahakama kuwa uchunguzi wa kesi hiyo umeshakamilika na kuiomba mahakama kutaja kusikilizwa kwa kesi hiyo mara baada ya vikao vya mahakama kuu vinavyotarajia kuanza mahakamani hapo wiki mbili zijazo jambo ambalo  upande wa washtakiwa ukiongozwa na wakili Bathromeo Tarimo kukubaliana na hoja hiyo  na kuungwa mkono na  hakimu anayesikiliza kesi Ivani Msaki hivyo kesi hivyo kuahirishwa hadi Februari ishirini na saba.

Watuhumiwa hao wanashtakiwa  kwa makosa nane ikiwemo kula njama ya kutenda kosa,kufanya mkusanyiko usio wa halali,kufanya ghasia,uchochezi wa kutenda kosa,kuchoma nyumba na mali ya serikali ya kijiji na uharibifu wa mali kwa makusudi makosa ambayo walitenda Novemba 26  katika uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika kata ya sofi wilayani Malinyi

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>