Published On: Tue, Jan 9th, 2018

Kigwangalla ateua kamati bonde la mto Kilombero

Share This
Tags

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla ameteua Kamati maalum ambayo itaishahuri Serikali namna ya nini kifanyike katika kushughulikia  athari za bonde la Kilombero lililopo Mkoani Morogoro.

Dk Kigwangalla amebainisha kuwa Kamati hiyo aliyoiteua,  ndio itamshauri juu ya bonde hilo litasimamiwa vipi pamoja na namna bora ya hatua za kuchukua ili kulinda bonde hilo ambalo lina mahitaji makubwa ikiwemo chanzo kikubwa  cha maji yanayotengeneza Stiegler’s Gorge ambako Serikali imeamua kuweka mikakati ya utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme unaotarajiwa kufikia megawatts 2100.

Kamati hiyo inaundwa na  wajumbe mbalimbali ambao wataongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Ndugu Andrew Napacho, Pia wajumbe ni  Brig. Gen. (Mst.) Edmund Mndolwa, Aliyekuwa Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Mstaafu Suleiman Kova, Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha wafugaji  Semkae Kilonzo (Policy Forum).

Wengine ni  Dk. Simon Mduma, Prof. Jaffar Kideghesho, Ruzika Muheto, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, MKuu wa Wilaya ya Kilombero,Mkuu wa Wilaya ya Malinyi,Mwenyekiti Halmashauri Ulanga, M/Halmashauri Kilombero, M/Halmashauri Malinyi  na M/Halmashauri Ifakara.

Pia yupo  Mtendaji Mkuu wa KPL, Mtendaji MKuu wa Illovo, Mkuu Kikosi JKT Chita. Wengine ni  Dk. Aggrey Mlimuka, Mwakilishi kutoka mamlaka ya maji Bonde la Kilombero, Mwakilishi kutoka Wizara ya ardhi.

Wajumbe wengine ni Ndugu.  Innocent Kylogeris, Dk. James Wakibara pamoja na Mkurugenzi Mkuu TAWA ambaye atakuwa Katibu wa Kamati hiyo.

Hatua hiyo inafuatia Dk Kigwangalla kufanya ziara maalum kwenye bonde hilo la kilombero ambapo ameweza kushuhudia athari kubwa zaidi zilizofanywa na wavamizi wakiwemo wakulima na wafugaji ambao wameonekana kuvamia maeneo makubwa  ndani ya pori tengefu la bonde pamoja na Kwenye eneo oevu ndani ya bonde hilo.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>