Published On: Wed, Jan 10th, 2018

Jinsi muziki unavyotumiwa kuongeza mazao ya nguruwe Rwanda

Share This
Tags

Mfugaji mmoja wa nguruwe kaskazini mwa Rwanda amepata siri ya aina yake kuwafanya nguruwe anaofuga kuongeza uzalishaji.

Siri hiyo ni muziki unaotumbuiza saa 24 katika mazizi yao.

Mfugaji huyo maarufu Sina Gerald anasema muziki huwasaidia nguruwe kunona, kujifungua vizuri na kutumia chakula kidogo ikilinganishwa na nguruwe wasiosikia muziki.

Mzee Theophile Hakizimana ambaye ni mpokezi ya wageni shambani anasema kuna aina mbili za nguruwe, Landras ambao ni nguruwe warefu na Large White ambao ni wafupi lakini wanono.

Ana nguruwe wapatao 700 pamoja na chakula cha kawaida , nguruwe hawa hupata muziki saa 24.

“Muziki huu unasaidia nguruwe kuwa watulivu,kuwa na afya nzuri,na pengine niseme kuwa nguruwe wanatoa uzalishaji mwingi wakati wanapata muziki kama huu” anasema Hakizimana.

Anasema kwa muda mrefu wamekuwa wakiendesha utafiti kuhusu nguruwe na uzalishaji wao kwa ujumla

Kuna pia faida kubwa kwa mfugaji kwa sababu Nguruwe wakipata muziki kama hivi wanakula chakula kidogo sana ukilinganisha na nguruwe ambao wanakula bila kusikia muziki.

“Hapa nalinganisha na chakula tunachowapa nguruwe wengine tulionao ambao wao hawapati muziki. Hii ni kwa mjibu wa utafiti tuliofanyia nguruwe katika kituo chetu”

Ufugaji wa nguruwe umeshika kasi nchini Rwanda kutokana na faida yake ya haraka kibiashara.

Nyama ya nguruwe ndiyo ghali kuliko nyama nyingine sokoni. Kilo moja ikiwa ni franga si chini ya elfu 4 za Rwanda kama dolla 5.

Kitoweo cha nguruwe ni miongoni mwa vitoweo vyenye mvuto wa hali ya juu kwenye vilabu vya pombe katika miji ya Kigali na Kampala kikifahamika kwa jina maarufu ”Akabenz”

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>