Published On: Wed, Jan 31st, 2018
World | Post by jerome

Bunge la Catalonia laahirisha uchaguzi wa rais

Share This
Tags

Spika wa bunge la jimbo la Catalonia Roger Torrent ameahirisha kikao cha bunge kwa muda usio julikana.

Bwana Torrent amechukua uamuzi huo baada ya mahakama ya juu ya Uhispania kuamua kwamba aliyekuwa rais wa jimbo hilo Carles Puigdemont hawezi kuchaguliwa tena bila ya yeye mwenye kuwapo bungeni.

Mahakama pia imeamuru kwamba lazima bwana Puigdemont apate ruhusa ya kushiriki katika shughuli za bunge kutoka kwa hakimu anayemchunguza kuhusiana na hatua yake ya kutangaza uhuru wa jimbo la Catalonia.

Hata hivyo bwana Puigdemont akizungumza kwa njia ya video amesema malengo yake yako pale pale na ametoa mwito kwa wabunge wanaounga mkono kujitenga kwa jimbo la Catalonia waendelee kusimama kwa pamoja.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>