BENK 5 ZAFUNGWA KWA KUSHINDWA KUTIMIZA MATAKWA
Benki kuu ya Tanzania imezifungia na kusitisha shughuli za kibenki kwa benki tano zilizokuwa zinafanyabiashara zake hapa nchini baada ya kushindwa kutimiza matakwa ya sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006.
Sheria ya mabenki na taasisi za kifedha ya mwaka 2006 inazitaka benki za jamii yaani community benki kuwa na mtaji unaofikia shilling billion 2 badala ya kiasi cha awali cha shilling million 200. Kufuatia uwepo wa sheria hiyo, benki kuu ilitoa muda wa miaka mitano kwa benki zote kuhakikisha zinafikia mtaji huo la sivyo zitakutana na mkondo wa sheria
Gavana wa Benki Kuu BENNO NDULU anaeleza hatua ambazo benki hiyo kuu imechukua dhidi ya benki ambazo hazijafikia matakwa hayo ya sheria.
Je kufungwa kwa benki hizo tano ambazo zina amana ya ujumla inayofikia shilling billion 67.8 sawa na asilimia 0.38 za amana zote nchini kuna athari gani kwa nchi
Profesa Ndulu pia amezungumzia kikomo cha malipo kwa wateja wa benki hizo ambazo walikuwa wameweka amana zao.
Clouds Tv imezungumza na baadhi ya wateja wa ilikuwa Njombe community bank na Kagera Farmers Cooperative bank na haya ndio maoni yao kuhusu kufungwa kwa benki hizo.