Published On: Tue, Dec 12th, 2017

Shughuli za binadamu zisifanyike msituni-Hasunga

Share This
Tags

Naibu Waziri wa wizara ya Maliasili  na Utalii  Japhet Ngailonga Hasunga ameutaka uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuhakikisha  shughuli zozote za Kibinadamu hazifanyiki Msituni na zoezi hilo lisiathiri ama kudhuru Binadamu waliokiuka Sheria  hizo kwani kazi kubwa ya Wakala wa huduma za misitu ni Uhifadhi.

Hasunga ametoa agizo hilo alipotembelewa  na Bodi ya ushauri ya Wizara ya maliasili na Utalii  kwa wakala wawa huduma za Misitu ambayo iliongozwa na Esther Mkwizu ambao waliwasilisha changamoto kubwa inayowakabili ya upungufu wa watumishi kwani kitaaalam afisa Misitu mmoja anatakiwa kuhifadhi hekta 500 za msitu wa asili wakati kwa msitu wa kupandwa afisa misitu mmoja anatakiwa kusimamia hekta 10,000 lakini kutokana na upungufu wawatumishi hivi sasa afisa misitu  mmoja anasimamia zaidi yahekta  10,000.

Katika hatua nyingine wajumbe wa Bodi wamemueleza naibu waziri huyo kwamba  Tanzania inayo fursa kubwa sana ya kufanya vizuri kwenye Mazao ya Nyuki ambapo kwa sasa ni nchi ya pili kwa Uzalishaji wa Asali katika Bara la afrika, huku ikitajwa kuwa na Mazao Bora ya nyuki ambapo soko lake katika Nchi za ulaya ni kubwa sana.

Alipokuwa akifanya Majumuisho Naibu waziri amewataka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Kuhakikisha wanabuni mbinu zitakazowezesha kumaliza migogoro ya Misitu na wananchi.

Hivi karibuni kumekuwa na Shughuli za kuondoa shughuli za Kibinadamu zinazoendelea kwenye Misitu ya Hifadhi ambapo utaalam unaonesha kwamba endapo shughuli hizo zikiachwa ziendelee kutakuwa na uharibifu wa vyanzo vyamaji, mzunguko wa hewa utaahiribiwa, Rutuba ya udongoitavurugwa jambo ambalo litaaathiri maisha ya binadamu mojakwa moja.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>