Published On: Mon, Dec 25th, 2017

Khloe Kardashian atarajia mwanawe wa kwanza

Share This
Tags

Nyota wa kipindi cha runinga, Khloe Kardashian amekuwa akiwaweka mashabiki wake katika hali ya eti eti kwa miezi kadhaa kuhusiana na iwapo anatarajia mtoto wake wa kwanza.

Usiku wa Jumatano , nyota huyo ambaye anachumbiwa na mchezaji wa mpira wa vikapu nchini Marekani NBA Tristan Thompson , aliweka picha isiyo na rangi ya tumbo lake kwenye mtandao wa Instagram: ”Tumepata mtoto.”

Khloe mwenye umri wa miaka 33 amesema wanandoa hao walitaka kufurahia habari hizo za”kibinafsi” kwa mara ya kwanza

Si mashabiki wengi watakaoshangazwa na habari hiyo, lakini mmoja wao alisema , ”hiyo ni habari njema.”

Kwenye chapisho lake , Khloe amesema ” ndoto yake kubwa imetimia”

Na akaendelea kumshukuru mpenzi wake , akisema .haamini kwamba mapenzi yao yangeleta kiumbe duniani.

”Tristan , asante kwa kunipenda jinsi unavyonipendaa, asante kwa kunihudumia kama malkia”.

”Asante kwa kunifanya kuwa mrembo katika kila sehemu. Trisan , asante kwa kunifanya mama.”

Habari hiyo njema inajiri mwaka mmoja baada ya Khloe kukamilisha talaka yake na mchezaji wa zamani wa mpira wa vikapu NBA Lamar Odom, ambaye aliolewa naye mwaka 2009 na kuachana baada ya miaka saba baadaye.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>