Published On: Thu, Nov 30th, 2017

WENYEVITI WA SERIKALI ZA VIJIJI WAONYWA KUBADILISHA MATUMIZI BORA YA ARDHI

Share This
Tags

Serikali imewaonya Wenyeviti wa Serikali za vijiji na Mitaa hapa nchini, kuacha tabia ya kubadilisha matumizi bora ya ardhi ili tu waweze kuchaguliwa katika nafasi za Uongozi wa kisiasa

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi,  amesema watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria hasa katika maeneo ambayo tayari Serikali imetumia fedha nyingi katika mipango hiyo.

Waziri Lukuvi amepiga marufuku hiyo akiwa wilayani Serengeti mkoani Mara, wakati akizungumza na wadau mbalimbali katika uzinduzi wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji 36 katika wilaya hiyo.

Lukuvi amesema ni marufuku kwa viongozi hao kubadilisha matumizi bila kushirikisha mkutano mkuu wa kijiji huku pia akiyataka mashirika ya uhifadhi kuheshimu mipango ya vijiji ili kuepusha migogoro ya ardhi isiyo ya lazima na Wananchi

Kwa mujibu wa Shirika la uhifadhi la Kimataifa la Frankfurt Zoological ambao limefadhili mpango huo wilayani Serengeti Shilingi bilioni 1.3 zinatarajiwa kutumika katika shughuli za upimaji pamoja na uandaaji wa matumizi bora ya ardhi.

Mpango huo utasaidia Sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kilimo na Mifungo kuwa na matumizi bora ya ardhi

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>