Published On: Wed, Nov 22nd, 2017

Waziri wa kilimo aagiza uongozi wa kiwanda cha katani kilosa kuwapa mikataba ya ajira wafanyakazi wake

Share This
Tags

Kufuatia malalamiko ya wafanyakazi wa kiwanda cha Katani cha China State Farms Agribusiness Corporation Tanzania Limited kilichopo wilayani Kilosa ya  kufanya kazi kwa muda mrefu bila mikataba ya ajira waziri wa kilimo Dr.Charles Tizeba ameagiza uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha unawapa mikataba ya ajira mara moja wafanyakazi hao.

Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho Asha Suleiman na Baraka Sihaba, wamesema wamefanya kazi kwa muda mrefu hadi kufikia  miaka kumi  kiwandani hapo lakini hawana mikataba ya ajira pamoja na kufanya kazi katika  mazingira magumu kutokana na kukosa vitendea kazi vinavyowalinda kiafya.

Kutokana na Malalamiko hayo waziri wa kilimo Dr Charles Tizeba akauagiza uongozi wa wilaya kupitia mkuu wa wilaya hiyo Adam Mgoyi, kuhakikisha anafuatilia suala hilo ili wafanyakazi wa kiwanda hicho cha Katani wapewe mikataba ya ajira na wale wa mashambani nao wapewe haki zao sambamba na kulindwa afya zao kwa kupewa vifaa vya kazi.

Waziri Dr Tizeba ametembelea mashamba ya miwa ya kampuni Tanzu ya Mkulazi yaliyopo eneo la Gereza la kilimo la Mbigiri  mradi unaoendeshwa na mifuko ya hifadhi ya jamii ya PPF na NSSF na kuuagiza  uongozi wa kampuni hiyo kuangalia namna ya kuwasaidia wakulima wa nje walioingia ubia na kampuni hiyo badala ya kuwaacha kuhangaika kutafuta mikopo kwenye taasisi nyingine za fedha.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>