Published On: Wed, Nov 29th, 2017

Watuhumiwa wa vurugu za uchaguzi mdogo Malinyi wafikia 43 .

Share This
Tags

Msako unaoendelea kufanywa na jeshi la polisi  mkoani Morogoro umefanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa wengine wawili  na kusababisha  idadi ya watuhumiwa wanaohusishwa na vurugu zilizojitokeza katika kata ya Sofi wilayani Malinyi wakati wa uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata hiyo, kufikia 43 huku mbunge wa jimbo la Kilombero Peter Lijualikali akiendelea kutafutwa.

Watuhumiwa wa vurugu hizo wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wameshafikishwa katika kituo kikuu cha Polisi mkoani Morogoro  baada ya kudaiwa  kuchomwa kwa  ofisi ya Mtendaji wa kata hiyo,darasa na nyumba ya mwalimu Novemba 25 na kwamba  miongoni mwa  watuhumiwa waliokamatwa ni pamoja na mbunge wa jimbo la Mlimba Susan Kiwanga.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro  SACP  Ulrich Matei amesema   watuhumiwa wote tayari wamefikishwa  katika kituo kikuu cha polisi mkoa  kwa ajili ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria baada ya upelelezi kukamilika.

Katika hatua nyingine Jeshi hilo linawashikilia watu wengine wanne  wanaotuhumiwa kusafirisha dawa za kulevya   aina ya bangi  katika maeneo tofauti  ndani ya Mkoa wa Morogoro.

Watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na polisi na baada ya upelelezi kukamilika  watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>