Published On: Tue, Nov 28th, 2017

Unajua kwa nini wanaume hawadensi?

Share This
Tags

Zaidi ya robo tatu ya wanaume nchini Uingereza wanasema hawajahi au aghalabu wao hudensi, kwa mujibu wa utaifiti wa YouGov survey uliofanyiwa wanaume 1,000 na BBC Radio 5 live.

Kigezo kikuu ni aibu – zaidi ya thuluthi ya wanaume waliohojiwa wanasema wanaona aiu kuingia uwanjani na kunengua viungo.

Asilimia 10 wanasema wanahofia kutazamwa wanapoingia sehemu ya burudani na kuanza kudensi , au kudhihakiwa au kuonekana hawajui kudensi.

Baadhi ya waliohojiwa wamekiri kuwa hufikiria sana kabla ya kuingia uwanjani au mara nyingine hulewa ili wajihisi vizuri na kujiamini.

“Sidhani kama najua kudensi na kwahivyo, huwa lazima nijipe ‘nguvu’kabla ya kuingia uwanjani kudensi,” alisema mmoja.

Gareth Dew, mwenye umri wa miaka 35, amekiri yeye hulewa ili apate kujihisi vizuri na kujiamini.

“Kawaida huwa silewi , lakini kama kuna hali ambapo ni lazima ni densi , lazima ninywe glasi kadhaa za whiskey kujituliza roho na kuondosha wasiwasi.”

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>