Published On: Tue, Nov 28th, 2017

Uchafuzi mkubwa wa bahari wasababisha viumbe wa bahari yenye kina kirefu kula plastiki

Share This
Tags

Hivi karibuni wanasayansi wamegundua nyuzi za plastiki kwenye utumbo wa viumbe wanaoishi katika bahari yenye kina kirefu, wakiwemo samaki wenye magamba wanaoishi katika mita elfu 11 chini ya bahari ya Pasifiki. Hali hii inaonesha kuwa hata bahari yenye kina kirefu imechafuliwa na takataka za binadamu.

Dr. Alan Jamieson kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle amesema viumbe wanaotegemea chakula kidogo wanaishi katika bahari yenye kina kirefu, lakini nyuzi za plastiki zilizotengenezwa na binadamu zimeingia kwenye mazingira hayo, na kusababisha viumbe wa huko kula nyuzi hizi.

Sampuli 90 za samaki wenye magamba zilikusanywa kutoka mifereji yenye kina kirefu katika bahari ya Pasifiki, ikiwemo mifereji ya Mariana, Japan, New Hebrides na Kermadec. Sampuli zilizokusanywa kutoka sehemu ya chini ya mfereji wa Mariana wenye kina cha mita elfu 11 zinaonesha kuwa karibu viumbe vyote vimekula vipande vya Nylon, Polyethylene na PVC.

Inakadiriwa kuwa hivi sasa tani milioni 300 za takataka za plastiki ziko baharini, na vipande zaidi ya trilioni 5 vyenye uzito wa tani laki 2 na elfu 50 vya plastiki vinaelea juu ya bahari. Dr. Jamieson alisema viumbe wengine wa baharini huenda pia wamekumbwa na uchafuzi wa nyuzi za plastiki.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>