Published On: Wed, Nov 29th, 2017
Sports | Post by jerome

Serikali ya DRC yawapa zawadi wachezaji TP Mazembe

Share This
Tags

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imewazawadia wachezaji wa klabu ya TP Mazembe fedha taslimu dola elfu tano kila mchezaji ikiwa ni motisha wa kuwapongeza kufuatia ushindi wa kombe cha shirikisho la soka Afrika ngazi ya klabu.

Akizungumza wakati wa kuwakabidhi fedha hizo, waziri wa michezo wa nchi hiyo, amesema uamuzi huo unatokana na timu hiyo kuitangaza vyema bendera ya taifa kwa kushinda mara mbili mfululizo kikombe hicho.

TP Mazembe imeshinda kombe la shirikisho kwa kuifunga Supersport United ya Afrika Kusini kwa jumla ya magoli 2-1 kwenye mechi za fainali.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>