Published On: Wed, Nov 29th, 2017
World | Post by jerome

Raila Odinga aapa kuapishwa kuwa rais wa Kenya mwezi Desemba

Share This
Tags

Kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Odinga, amekataa kuutambua utawala wa Rais Uhuru Kenyatta na kusema ataapishwa kama rais wiki mbili kutoka sasa.

Odinga amesema sherehe za kuapishwa zitafanyika Desemba 12, ikizilinganisha sherehe hizo na zile za kuapishwa rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, baada ya Robert Mugabe kung’olewa madarakani.

Rais Kenyatta aliapishwa rasmi jana kuhudumu muhula wa pili na wa mwisho madarakani, baada ya kushinda uchaguzi mpya uliofanyika Oktoba 26 na uliosusiwa na Odinga.

Uchaguzi wa rais wa Agosti ulifutiliwa mbali na Mahakama ya Juu kutokana na dosari katika shughuli ya kuhesabu na kutangaza matokeo.

Kenyatta ameahidi kuliunganisha taifa la Kenya ambalo limegawika vibaya kutokana na tofauti za kisiasa.

Watu wasiopungua watatu waliuawa na polisi huku mzozo wa kisiasa ukiendelea kuikumba Kenya.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>