Published On: Tue, Nov 7th, 2017

Kituo cha kwanza cha kuzalisha umeme kisichotoa hewa ya Carbon Dioxide duniani

Share This
Tags

Baada ya kujenga kiwanda cha Direct Air Capture DAC ambacho ni cha kwanza kuweza kuvuta Carbon Dioxide kutoka hewani, Kampuni ya Climeworks ya Uswisi imepiga hatua mpya tena, ambayo imejenga kituo cha kwanza cha kuzalisha umeme kisichotoa hewa ya Carbon Dioxide duniani kwa kushirikiana na kituo cha kuzalisha umeme kwa maji ya moto nchini Ireland.

Katika miaka ya hivi karibuni, kikundi cha mradi wa CarbFix kinachoundwa na wanasayansi kutoka nchi mbalimbali kimekuwa kinatafuta njia ya kubadilisha hewa ya Carbon Dioxide kuwa madini. Wanasayansi hao wameingiza Carbon Dioxide kwenye maji, halafu kupeleka maji hayo kwenda mita 700 chini ya ardhi kwa mabomba. Hewa hiyo iliyoko kwenye maji ikikutana na miamba aina ya Basalt inabadilika kuwa madini ya Carbonate.

Kabla ya hapo, wanasayansi walifikiri mchakato huo unahitaji mamia hadi maelfu ya miaka, lakini mwandishi mkuu wa mradi wa CarbFix Dr. Juerg Matter amesema utafiti unaonesha kuwa asilimia 95 hadi 98 ya Carbon Dioxide yanabadilika kuwa madini kwa miaka miwili tu.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Climeworks Bw. Christoph Geblad amesema teknolojia hii ina mustakabali mzuri, kwa sababu miamba aina ya Basalt iko katika sehemu nyingi duniani licha ya Ireland, na teknolojia hii ikikomaa na kutumiwa katika sehemu nyingi, Carbon Dioxide itabadilika kuwa madini na kulimbikizwa chini ya ardhi ndani ya muda mfupi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>