Published On: Fri, Nov 3rd, 2017

KATIKA KUPUNGUZA MIMBA ZISIZOTARAJIWA KWA VIJANA WAKIKE IMESHAURIWA VIJANA WA KIUME KUWA NA STADI ZA MAISHA

Share This
Tags

 

Katika kupunguza mimba zisizotarajiwa kwa vijana wakike ,Imeshauriwa vijana wa kiume kuwa na stadi za maisha ili kuwafanya kujitambua na kuchakarika zaidi na shughuli za kujipatia kipato ambazo zitawajenga kiuchumi na kutoyapa kipaumbele masuala ya ngono Zembe.

Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto ni miongoni mwa sehemu muhimu ya Mpango wa Taifa wa Afua Muhimu za Afya ya Uzazi na Mtoto (NPERCH) unaozingatia kuimarisha ubora wa maisha ya wanawake, vijana balehe na watoto.

Kwakawaida Vifo vya Uzazi mara nyingi husababishwa na vipengele vinavyohusika na ujauzito, kujifungua na huduma za afya zisizoridhisha,hapa ndipo dhana ya uzazi wa mpango inapoibuka na kuwa mwarobaini wa kupunguza vifo vya akinamama.

Uboreshaji wa huduma za Afya, kupitia utafiti na majadiliano yanayolenga kuibua mawazo mapya ni mambo yasiyoepukika ili kufikia ubora katika sekta ya Afya kama wanavyoeleza waandaji wa mkutano wa kimataifa wa masuala ya afya .

UZAZI wa mpango ni uamuzi wa hiari unaofanywa na mtu binafsi, wanandoa au wenzi walio nje ya ndoa ambao hupanga ni lini wapate watoto, idadi wanayoitaka na baada ya muda gani.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>