Published On: Wed, Nov 29th, 2017

IGP Sirro aahidi kupambana na wimbi la wahamiaji haramu.

Share This
Tags

Mkuu wa jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro ameahidi kulivalia njuga suala la wimbi la wahamiaji haramu ambao wamekuwa wakiingia nchini kinyemela hali ambayo inachangia  kwa kiasi kikubwa  kuwepo kwa uvunjifu wa amani kwani baadhi yao wanashiriki katika mitandao ya ugaidi, ujamabazi na uingizaji wa madawa ya kulevya.

Sirro ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Pwani ambapo amekutana na maafisa mbalimbali wa jeshi hilo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa lengo la kujadili changamoto mbali mbali zinazohusiana na masuala ya ulinzi na usalama ili kuweka mikakati ambayo itaweza kusaidia katika kupunguza matukio ya uhalifu  na mauaji ambayo yamekuwa yakijitokeza katika Wilaya za Kibiti,Mkuranga na Rufiji.

Aidha IGP Sirro amesema kwa sasa matukio ya uhalifu katika Mkoa wa Pwani yameweza kupungua kwa kiasi kikubwa kutokana na kufanikiwa kuwakamata baadhi ya watu waliokuwa  wanajihusisha na matukio mbalimbali  ya mauaji pamoja na kukamata silaha ambazo walizichukua kwa askari polisi ambao walikuwa wakitekeleza majukumu yao.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Jonathan Shanna akazungumzia changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vitendea kazi vya kutosha ikiwemo magari, uhaba wa vituo vya polisi na nyumba kwa ajili ya kuishi askari.

Naye Sheikh mkuu wa Mkoa wa Pwani Hamisi Mtupa amempongeza Mkuu wa jeshi la Polisi nchini kwa juhudi za kuweza kurejesha hali ya amani katika maeneo ya Wilaya za Mkuranga,Rufiji, pamoja na Wilaya mpya ya Kibiti, kwani awali kulikuwa na machafuko ambayo yalisababisha hata kushughuli za maendeleo kwa wananchi kusimama.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>