Published On: Sat, Nov 25th, 2017

HISTORIA NYINGINE YA FIESTA KUANDIKWA LEADERS LEO

Share This
Tags

Msimu wa Tigo Fiesa unafikia kilele leo jijini Dar es salaam.

Tayari watu wapenda burudani walishaanza kusogea katika viwanja vya leaders Club kwa ajili ya kushuhudia msimu huo ambao kwa mwaka huu utaandika tena historia nyingine.

Kilele cha msimu huu kimekuja kwa aina nyingine ambapo wasasanii wa hapa nyumbani ndio watakaotumbuiza tofauti na ambavyo imekuwa kwa miaka ya nyuma.

Waratibu wa tamasha hilo wameeleza kwamba nia kubwa ya kufanya hivyo ni kuwapa nafasi zaidi wanamuziki wa nyumbani kwa kuzingatia uzalendo, kwani wamejipanga, na kiwango chao hakina tofauti na wale ambao hutoka nje.

Wasanii bora wa kike kwa kiume watalipamba jukwaa la msimu wa Togo Fiesta usiku wa leo.

Viongozi mbalimbali wa serikali pia wanatarajiwa kuwa sehemu ya kilele cha msimu huo, bila kuwasahau waigizaji wa filamu nchini.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>