Published On: Tue, Oct 24th, 2017

Wanafunzi kutoa elimu kuhusu imani potofu

Share This
Tags

Wanafunzi wa shule ya sekondari DUTWA  wilayani Bariadi  mkoani Simiyu wameahidi  kutoa elimu kwa  jamii ili iachane na mila potofu  kuwa viungo vya mtu mwenye ualbino vinaleta utajiri.

Wanafunzi hao wamebainisha hayo katika mkutano uliowashirikisha waganga wa kienyeji, wananchi mbalimbali na wanafunzi hao kwa lengo la kuhamasisha jamii kutokomeza mauaji ya watu wenye ualbino chini ya uratibu wa asasi ya Mass Media Bariadi.

Katika kampeni hiyo wanafunzi hao wameahidi kushirikiana na Asasi ya mass media Bariadi kuhakikisha wanatoa elimu na hatimaye jamii iweze kubadilisha mtazamo juu ya mauaji ya watu wenye ualbino.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Dutwa amewapongeza wanafunzi hao kwa kushiriki kampeni hiyo na kuwataka kuendeleza jitihada hizo katika kutokomeza imani potofu katika jamii.

Nao baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka taasisi ya mass media Bariadi na kutoka jeshi la polisi wilayani humo wameelezea umuhimu wa kampeni hiyo inayofanyika katika wilaya tatu za mkoa wa Simiyu.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>