Published On: Tue, Oct 24th, 2017

Serikali yatakiwa kuboresha miundombinu ya gereza la wilaya Geita.

Share This
Tags

Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constatine Kanyasu ameiomba Serikali kuboresha miundombinu ya Gereza la Wilaya ya  Geita ambalo limejengwa enzi za Mkoloni ili kuepukana na mrundikano wa wafungwa na mahabusu gerezani na kuhatarisha usalama wa afya zao.

Kanyasu ametoa kauli hiyo baada ya kuwatembelea wafungwa na mahabusu kwa ajili ya kuwapatia misaada mbalimbali ikiwemo sabuni na sukari, ambapo amejionea ufinyu wa magereza hiyo ambayo ina uwezo wa kuchukua watu 170 lakini kwa sasa inahudumia zaidi ya watu 500.

Kwa upande mwingine uongozi wa Gereza hilo umepokea msaada wa gari aina ya LAND CRUSIER kutoka kwa mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM).

Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) umekuwa ukisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo na katika gereza la Wilaya ya GEITA ambapo mwaka huu walitoa vifaa vya kukarabati mfumo wa maji taka na kipindi hiki wametoa msaada wa gari.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>