Published On: Tue, Oct 24th, 2017
World | Post by jerome

EU yaahidi mamilioni kuwasadia wakimbizi wa Rohingya

Share This
Tags

Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, imeahidi kuchangia kiasi cha euro milioni 30 zaidi, katika msaada kwa mamia kwa maelfu ya Waislamu wa Rohingya waliokimbia ukandamizaji Myanmar na kutafuta hifadhi nchini Bangladesh.

Umoja wa Ulaya umetoa ahadi hiyo katika mkutano wa kuchagisha fedha wa Umoja wa Mataifa uliofanyika mjini Geneva, Uswisi unaolenga kukusanya misaada yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 400, kufikia Februari mwakani.

Mpaka sasa karibu dola milioni 350 zimeahidiwa na serikali za mataifa na wafadhili wa kimataifa. Umoja wa Mataifa umeitaja michago hiyo kuwa hatua ya kutia moyo kueleka kuwasaidia karibu wakimbizi milioni moja wa Rohingya, wanaoishi katika kambi za muda nchini Bangladesh.

Wakati huo huo, Marekani imesema inazingita kuiwekea vikwazo Myanmar, kuhusiana na vurugu dhidi ya Warohingya, ikisema katika taarifa kuwa mtu yeyote au taasisi zinazohusika na ukatili dhidi ya jamii hiyo zitawajibishwa.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>