Published On: Tue, Oct 10th, 2017

Chui aliyesimamisha shughuli katika kiwanda cha magari India akamatwa

Share This
Tags

Maafisa wa wanyajapori wamemkamata chui baada ya karibu saa 36 tangu aonekane mara ya kwanza ndani ya kiwanda cha magari.

Waokoaji walimdunga dawa ya kumtuliza myama huyo baada ya oparesheni kubwa ya kumsaka ndani ya kiwanda cha magari ya Maruti Suzuki kilicho mji wa Manesar, usio mbali saana na mji mkuu Delhi.

Chui huyo mara ya kwanza alionekana siku ya Alhamis asubuhi kupitia Camera za CCTV na kuonekana tena mara kadhaa baadaye.

Wafanyakazi wa usiku waliondolewa kutoka jenge hilo na sehemu ya kuwanda hicho kikubwa kufungwa.

Kiwango hicho ndicho kikubwa a zaidi nchini India kinachounda karibu magari milioni 1 kwa mwaka.

Wakati maelfu ya wafanyakazi waliwasili asubuhi, waliambiwa kusubiri njee wakati maafisa 12 wa misitu na karibu polisi 50 walitumwa kumwinda chui hiyo.

Mnyama huyo alionekana kupitia kamera CCTV katika idara ya injini iliyo na karibu ukuwa wa ekari 6.

Mwandishi mmoja wa habari katika eneo hilo aliiambia BBC kuwa waokoaji walileta mbuzi wawili waliokuwa hai na nyama mbichi ili chui huyo aweze kutoka mafichoni.

Lakini baada ya chui hiyo kutafutwa na kudunngwa dawa ya kumtuliza alishikiwa na kupelekwa kupewa matibabu kabla ya kurudishwa porini.

Visa vya makabiliano kati ya ya binadamu na wanyama vimekuwa vingi nchini India, ambapo makao ya wanyamapori yanazidi kudidimia na kuchangia ndovu na chui kuingia maeneo ya watu.

Kuna takriban chui 12,000-14,000 nchini humo na takriban mmoja huuliwa kila siku.

Mwaka uliopita chui aliingia kwenye shule moja iliyo mji wa Bangalore nchini India, na kuwajeruhi watu 6 ambao walijaribu kumkamata

Ilichukua muda wa saa kumi kumdunga dawa ya kumtuliza na kumkamata chui huyo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>