Published On: Wed, Sep 13th, 2017

Wizi wa mafuta na vifaa vya ujenzi washamiri Mtwara.

Share This
Tags

Jeshi la polisi mkoani Mtwara limesema kumeibuka tabia ya wizi wa mafuta katika viwanda vya Saruji vya Dangote na Mtwara Cement, pamoja na wizi wa vifaa vya ujenzi katika kampuni zinazojenga barabara mkoani humo.

Akizungumaza mkoani humo, kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Naibu Kamishna wa Polisi Lucas Mkondya, amesema tayari wamegundua kuwa ni wizi wa kimtandao unawahusisha baadhi ya waajiriwa katika viwanda na kampuni hizo wanaoshirikiana na raia pamoja na kampuni za ulinzi.

Kamanda Mkondya akatoa onyo kwa wafanyakazi wa viwanda hivyo, makampuni ya ulinzi pamoja na mameneja wao kukomesha tabia hizo kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Katika hatua nyingine, jeshi hilo linawashikilia watu Watano ambao wanadaiwa kuhusika na tukio la kumshambulia kwa silaha hakimu wa mahakama ya wilaya ya Masasi Khalfan Ulaya na kumsababishia kifo kilichotokea Septemba 8 mwaka huu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Jeshi hilo bado linaendelea na msako ili kuwatia nguvuni wahalifu wengine waliohusika na tukio hilo lililotokea Agosti 14 mwaka huu wilayani Masasi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>