Published On: Tue, Sep 12th, 2017

Waziri mkuu Aahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini

Share This
Tags

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi ambaye ameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu ujao.

Amekutana nae leo kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam na amesema tayari Serikali imeanza kuwahamasiha wakulima kuongeza uzalishaji kwa kuwa kuna soko la uhakika.

Waziri Mkuu amempongeza Bw. Pardesi kwa kuiunga mkono Serikali katika mpango wake wa kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda.

Kampuni ya Namera Group of Industries inamiliki kiwanda cha nguo cha NIDA na cha Namera vya jijini Dar es Salaam na inatarajia kufungua kiwanda kingine cha nguo wilayani Kahama.

Kwa upande wake Bw. Pardesi amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba kampuni yao ina uwezo wa kununua pamba yote inayozalishwa nchini na kuichakata katika viwanda vyao na kutengeneza nguo zitakazouzwa nchini kwa bei nafuu.

Amesema kwa sasa wameajiri mafundi katika viwanda vyao ambao watakuwa wanashona nguo na kuziuza nchini kwa gharama nafuu ili kuwawezesha wananchi wa hali ya chini kumudu kununua na kuondokana na matumizi ya nguo za mitumba.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>