Published On: Sat, Sep 9th, 2017
World | Post by jerome

Watu 60 wafa Mexico kwa tetemeko la ardhi

Share This
Tags

Mexico imetangaza siku tatu za maombolezo, baada ya moja ya matetemeko makubwa kabisa kuwahi kutokea kulikumba eneo la kusini mwa nchi hiyo, likiyaangusha majengo na kuangamiza maisha ya watu zaidi ya 60.

Tetemeko hilo lililopiga usiku wa kuamkia Ijumaa (8 Septemba) lilikuwa kubwa mno kiasi cha kwamba hata majengo imara katika mji mkuu, Mexico City, yalitikisa, yakiwa umbali wa kilomita 1,000 kutoka kilipo kitovu cha tetemeko lenyewe.

Rodrigo Soberanes, anayeishi karibu na San Cristobal de las Casas jimbo la Chiapas lilikotokea tetemeko hilo anasema nyumba yake “iliyeyuka kama ubani wa kutafuna.”

Tetemeko hili limeikumba Mexico wakati ikiwa inapambana na madhara ya Kimbunga Katrina upande mwengine wa nchi. Mvua kubwa zimeripotiwa kwenye jimbo la Veracruz, ambako upepo mkali wa Kigawe 2 ulitarajiwa kuzidi Ijumaa jioni au mapema Jumamosi.

Rais Enrique Pena Nieto alisema kuwa watu 61 wamekufa kutokana na tetemeko hilo – 45 katika jimbo la Oaxaca, 12 Chiapas na 4 Tabasco. Mji ulioharibiwa zaidi ni Juchitan, ambako watu 36 walikufa. Nusu ya mji huo umegeuzwa kifusi na mitaa imejaa mabaki ya nyumba za raia.

Hospitali moja pia ilianguka, kwa mujibu wa Rais Pena Nieto aliyetembelea mji huo na kukutana na wakaazi wa huko. Wagonjwa wamehamishiwa maeneo mengine.

Rais huyo alisema kuwa mamlaka zinashughulikia kurejesha huduma ya maji na chakula na kutoa matibabu kwa wale wanaohitaji. Aliahidi kuwa serikali yake ingeliwasaidia waathirika kujijenga upya, huku akitoa wito wa umoja.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>