Published On: Sat, Sep 9th, 2017

WATANZANIA WAOMBWA KUMUOMBEA LISSU

Share This
Tags

Chama cha Demokrasia na maendelo CHADEMA mkoani Mara kimewataka wananchama wake na watanzania kiujumla kuungana pamoja kumuombea mbunge wa singida mashariki na mwanasheria mkuu wa chama hicho  Tundu Lissu ili aweze kureja kuwatumikia waananchi .

Kufuatia tukio la kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana

Tundu Lissu ambae pia ni Rais wa chama cha mawakili wa Tanganyika (TLS ) Taifa , hivi karibuni alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana

Awali akizungumza mkoani Mara kaimu mwenyekiti Chadema Chacha Heche, ambae ni katibu wa chama hicho mkoa mara, akaitaka serikali kuwaimarishia ulinzi wabunge ili kuondokana na hofu iliyotanda miongoni mwao .

Akieleza Dhamira ya chama kwa niaba ya wanachama wa Chadema, katibu wa chama hicho wilaya Tarime Thobias Ghati amewasihi viongozi wa serikali kuwabaini waliohusika na kitendo hicho cha shambulio kwa mbunge Tundu Lissu kwani bado ni tegemeo kubwa kwao .

Wananchama hao pamoja na viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Mkoani Mara wameungana na wenzao nchini kote kumuombea dua Tundu Lissu ili mungu amsaidie aweze kurejea katika hali yake ya kawaida na kuweza kuwatumikia watanzania kwa ujumla .

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>