Published On: Wed, Sep 13th, 2017

Wanne mbaroni kwa uporaji pikipiki

Share This
Tags

Jeshi la Polisi Mkoani Tabora,limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne waliokuwa kwenye mtandao wa uporaji Pikipiki, na kuwataka waendesha bodaboda kulisaidia jeshi hilo kwa kuchukua tahadhari ili wasifikiwe na matukio ya kuporwa Pikipiki zao pamoja na kuuawa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroad Mutafungwa,akitoa taarifa  baada ya kuwakamata watu hao anasema waendesha bodaboda wanaweza kuwa msaada mkubwa kwa kuchukua tahadhari.

Pia amewataka kutoa taarifa kuhusiana na wateja wanaowatilia mashaka wanapowasafirisha ili hatua ziweze kuchukuliwa kabla ya madhara kutokea.

MAGANGA HARUNA ,WAZIRI KIPUSI  na ALLY HAILALA ni baadhi ya waendesha bodaboda wamelipongeza  jeshi la Polisi kwa kuwakamata watuhumiwa wa upoaraji pikipiki.

Zaidi ya waendesha bodaboda kumi wameuawa na zaidi ya kumi na moja kuporwa Pikipiki katika matukio yaliyotokea kipindi cha miezi kumi na nane iliyopita Mkoani Tabora.

 

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>