Published On: Sat, Sep 9th, 2017

WAKUU WA MIKOA 10 WAAGIZWA KUSIMAMIA PAMBA

Share This
Tags

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa mikoa 10 inayolima pamba nchini wasimamie zao hilo kwa karibu ili kuinua uzalishaji wake na kuwaongezea kipato wananchi.

Waziri Mkuu ametoa agizo wakati akizungumza na wakuu hao wa mikoa kwenye kikao alichokitiisha mjini Dodoma kujadili mbinu za kufufua zao hilo.

Wakuu wa mikoa walioitwa kwenye kikao hicho ni kutoka mikoa ya Shinyanga, Singida, Kagera, Tabora, Morogoro, Mara, Mwanza, Simiyu, Katavi na Geita.

Waziri Mkuu alisema Serikali imeamua kusimamia kilimo cha pamba kuanzia maandalizi ya shamba, kupanda, matumizi ya pembejeo na dawa, kuvuna na kutafuta masoko na akawataka wasimamie katika maeneo yao ili kilimo cha zao hilo kiweze kubadilika.

“Ni lazima kila mmoja awe na mpango kazi, ausimamie na atoe matokeo ya kuwa zao hili limefanikiwa katika eneo lake. Tunataka zao hili lichukue nafasi yake ya namba moja. Heshima ya “Dhahabu Nyeupe” lazima irudi lakini pia ni vema mkumbuke kuwa zao la pamba ni uchumi, zao la pamba ni siasa katika mikoa yenu,” alisisitiza.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>