Published On: Wed, Sep 13th, 2017
Business | Post by jerome

Wafanyabiashara Njombe wafunga maduka kuwakwepa TRA

Share This
Tags

Wafanyabaishara katika mji wa Makambako Mkoani Njombe wamefunga maduka na soko kuu la mji huo wakiitaka Serikali kusitisha zoezi la ufungaji maduka yasiyotumia mashine za kielekronic za kukatia risiti EFDs huku wakiomba mashine hizo zigawiwe bure kama ilivyofanyika kwa baadhi ya wafanyabiashara jijini Dar es salaam.

Zaidi ya Maduka 90 yameonekana Kufungwa huku maeneo yaliyoonekana Kuathirika Zaidi ni Stand ya Zamani, soko kuu na Stand Mpya.

Wakizungumzia Uamuzi huo wafanyabiashara hao wanasema hawapingi Mpango wa serikali wa kutumia mashine hizo bali wanachokitaka ni Serikali kuwapa Mashine hizo Bure kama ilivyofanya Jijini Dar Es Salaam.

Pamoja na baadhi ya wafanyabiashara kutekeleza agizo hilo la kununua mashine,Miongoni mwao wamelalamikia kutapeliwa na Makampuni yaliyoingia Mkataba wa kusambaza mashine hizo.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akatoa siku 40 kwa wafanyabiashara hao kununua mashine za kukatia risiti vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>