Published On: Mon, Sep 11th, 2017
Sports | Post by jerome

WADAU MBALIMBALI WA MPIRA WA MIGUU ILI KUJADILI WATAKAVYOENDESHA MASHINDANO YA NYANZA CUP

Share This
Tags

Serikali Mkoani Geita imesema ilivunjika moyo wa kuiunga mkono soka la mpira wa miguu baada ya timu ya Geita Gold Sports  ya Mkoani humo kushushiwa rungu la adhabu katika michuano ya ligi daraja la kwanza  katika msimu wa 2015/2016 kwa  kile kinachoelezwa walipanga matokeo na timu ya kanembwe JKT ya Mkoani Kigoma ili kujipatia tiketi ya kufuzu Ligi kuu Tanzania Bara.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita HERMAN KAPUFI kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Meja Jenerali Mstaafu EZEKIEL KYUNGA walipokutana na wadau mbalimbali wa mpira wa miguu ili kujadili namna watakavyoendesha mashindano ya Nyanza Cup ambayo yamelenga kuibua vipaji vya wachezaji.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema kwa sasa wanaanzisha vuguvugu jipya la kimichezo chini ya chama cha soka Mkoa wa Geita GEREFA.

Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Geita (GEREFA) DEUS SEIF amesema kuanzishwa kwa mashindano ya Nyanza Cup ni kuwaweka sawa katika michuano ya hapo badae.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>