Published On: Mon, Sep 4th, 2017
Business | Post by jerome

VIJANA WENYE ULEMAVU WAPEWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI ARUSHA

Share This
Tags

Dhamira ya Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha Tanzania ya Viwanda inatimia, na vijana wanapewa nafasi kubwa ya kutekeleza azma hiyo ya Serikali.

Katika kiwanda kidogo cha SHANGA kilichopo jijini Arusha wamekusanywa vijana mbalimbali wenye ulemavu wakipatiwa mafunzo ya namna ambavyo wanaweza kutumia malighafi za kawaida kutengeneza bidhaa mbalimbali kama vile nguo, shanga, mazulia na baadhi ya vyombo vya majumbani.

OMARY JUMANNE ni mwanafunzi aliyefika katika kiwanda hicho ambaye anasema ameanza kuona mwanga wa maisha yake.

ABUU MACHUMU ni mwalimu mwenye miaka 13 kwenye kazi hiyo ya kufundisha vijana ambaye ameweza kuwasaidia vijana wengi kupata ujuzi.

Ameongeza pia kwamba ili kiwanda hicho kidogo kiweze kuendelea ni lazima pawepo uungwaji mkono mkubwa wa serikali.

Hii ni miongoni mwa shughuli inayosaidia kupunguza tatizo sugu la ajira katika jiji la Arusha ambalo mwishoni mwa juma hili litaweka historia ya kuuzindua msimu wa TIGO FIESTA 2017 na kabla ya tukio hilo Msimu wa TIGO FIESTA utaendelea kukuonyesha fursa mbalimbali zinazopatikana katika mkoa huo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>