Published On: Tue, Sep 26th, 2017
Science | Post by jerome

Uwezo wa kutambua nyuso si hulka

Share This
Tags

 

Kwa nini ni vigumu kwa baadhi ya watu kutofautisha nyuso tofauti huku wengine wanatofautisha vizuri? Wanasayansi wengi walifikiri binadamu na nyani wana hulka ya kutambua nyuso, wamepata uwezo huo tangu wazaliwe. Lakini utafiti mpya uliofanywa na watafiti wa Marekani unaonesha kuwa uwezo huo unapatikana baada ya kufanya majaribio mengi.

Watafiti wa Chuo Kikuu cha Harvard cha Marekani wamesema ili kujua jinsi binadamu na nyani wanavyopata uwezo wa kutambua nyuso, wamefanya majaribio kwa kima. Wamegawanya kima kwenye vikundi viwili. Kima wa kikundi cha kwanza wanalelewa kwa njia ya kawaida, wanaishi pamoja na mama, kima wengine na binadamu tangu wanapozaliwa. Kima wa kikundi cha pili wanatenganishwa na mama zao na kima wengine tangu wanapozaliwa, na wanalelewa na binadamu wanaovaa mask ili wasione nyuso za kima au binadamu.

Baada ya kufanya majaribio hayo kwa siku 200, watafiti walipima sehemu zinazofanya kazi za kutambua nyuso, mikono, vitu na mahali kwenye ubongo wa kima kwa kifaa cha MRI, na kugundua kuwa sehemu inayofanya kazi ya kutambua nyuzo imekua vizuri kama sehemu za kutambua vitu vingine kwenye ubongo wa kima wa kikundi cha kwanza, lakini ubongo wa kima wa kikundi cha pili unakosa sehemu ya kutambua nyuso. Na kima wa kikundi cha kwanza wanapenda kutazama nyuso kwenye picha za binadamu au nyani, na wale wa kikundi cha pili wanapenda kutazama mikono.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>