Published On: Tue, Sep 12th, 2017

Ufuatiliaji wa Miradi ya Umma.

Share This
Tags

Katika jitihada za kuleta maendeleo kwenye jamii ,upo umuhimu wa wananchi kutambua na kufuatilia miradi ya umma inatekelezwa kikamilifu katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuzingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu ili kuhakikisha  huduma zinawafikia  walengwa bila kujali maumbile yao.

Akiongea mara baada ya kukabidhi taarifa ya ufuatiliaji wa miradi ya umma kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Migara halmashauri ya Bukoba,Mwenyekiti wa kamati ya ufatiliaji rasilimali za umma iliyoundwa na chama cha wasioona (TLB )kupitia mradi wa ufuatiliaji  rasilimali na fedha za umma  ( PETS) amesema miradi mingi hasa ofisi na shule zimejengwa bila ya kuzingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho amesema kuwa utaratibu wa ufuatiliaji miradi inayotekelezwa katika kijiji, itasaidia kuongeza ufanisi wa utendaji kazi, kudhibiti ubadhirifu  wa miradi pamoja na kusimamia majengo ya umma yanayojengwa yazingatie  mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu.

Kwa upande wake mratibu wa mradi huo wa ufuatiliaji wa rasilimali na fedha za umma (PETS) amesema mradi huo umelenga kutoa uelewa kwa wananchi ili waweze kujua na kutambua miradi inatekelezwa kwa kiwango kilichokusudiwa  na inazingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>