Published On: Fri, Sep 8th, 2017

TEMBO WAHARIBU HEKA 10 ZA MAZAO WANANCHI WALIA HAWANA CHAKULA TENA.

Share This
Tags

Wakazi wa Kijiji cha Sora Kata ya Endakiso Wilayani Babati Mkoani Manyara wameingiwa na Hofu baada ya Tembo kuvamia Kijiji hicho na kumaliza mbaazi iliyo tayari kuvunwa.

Mmoja wa wakazi hao Hamisi Suleiman amesema Tembo wamemaliza ekari zake kumi ambazo ndio zilikua Tegemeo lake baada ya mavuno auze ili aweze kuendesha maisha yake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Sora Iddi Salim amesema Tembo hao wamesababisha kero kwao na hasara kubwa kwa wananchi.

 

Akiongea kwa njia ya Simu Stephano Koli ambae ni Muhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya taifa ya Tarangire inayopakana na kijiji hicho  alisema idara ya wanayama pori ndio inahusika na hilo swala ila wao husaidia tu kwenda kufukuza tu wanyama hao wasifanye uharibifu zaidi.

Hifadhi ya Taifa ya Tarangire imepakana na Vijiji vya Soraa na Endakiso ambavyo wakazi wake ni wakulima hivyo kila mwaka wanakabiliana na uvamizi wa Tembo kipindi cha mavuno kutokana na hali ya ukame ambao unawalazimu wanyama hao kutafuta malisho na maji.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>