Published On: Tue, Sep 12th, 2017
Business | Post by jerome

StarTimes kuzindua huduma bure za televisheni ya kidijitali kwenye maeneo ya vijijini Afrika

Share This
Tags

Kampuni ya televisheni ya China StarTimes inapanga kuzindua huduma za matangazo ya TV ya kidijitali bila malipo kwenye sehemu za vijijini barani Afrika, ikiwa ni sehemu ya majukumu yake ya kijamii.

Mkurugenzi Masoko na Uhusiano wa kampuni hiyo Bw. Japheth Akhulia amesema mradi huo utanufaisha vijiji 10,000 barani Afrika. Kwa sasa StarTimes imekuwa sehemu muhimu ya jamii ya Afrika, na hivyo inahitaji kuchangia katika kuendeleza jamii kwa kuboresha hali yao ya maisha.

Hivi sasa StarTimes inafanya mazungumzo na maofisa wa serikali za nchi mbalimbali za Afrika ili kutafuta njia ya kuhakikisha utekelezaji wa mradi huo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>