Published On: Fri, Sep 8th, 2017

SPIKA AAGIZA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA KUKUTANA KUJADILI MATUKIO YA UTEKWAJI

Share This
Tags

Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania JOB NDUGAI ameiagiza kamati ya kudumu ya bunge ya ulinzi na usalama kukutana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kupata taarifa juu ya maswala yanayoendelea ya watu kutekwa na kufanyiwa mashambulizi mbalimbali.

Spika wa bunge amefikia hatua hiyo baada mbunge wa Nzega Mjini HUSSEN BASHE kuomba kamati hiyo kufanya uchunguzi na kuleta bungeni taarifa kuhusu matukio hayo ikiwemo tukio la mbunge wa Singida Mashariki kupigwa risasi nyumbani kwake.

Bashe amesema kuwa kwa sasa wabunge wamekuwa hawana uhakika na usalama wao hivyo jambo hilo ni vyema likapelekwa kwenye kamati hiyo na taarifa hiyo ipelekwe bungeni.

Spika wa Bunge wakati  akitoa muongozo huo akaitaka kamati hiyo kukutana kama jinsi mh BASHE alivyoomba mwongozo na kuwasilisha taarifa hiyo kabla ya bunge kumalizika september 15 mwezi huu.

Awali spika NDUGAI amesema sababu za mh TUNDU LISSU kwenga kutibiwa nchini Kenya ni kutokana na maombi ya familia yake na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni  FEEMAN MBOWE na sio sababu zinazo sambazwa katika mitandao ya kijamii na hali ya mbunge huyo inaendelea kuimarika.

Baadhi ya wabunge wakaelezea jinsi walivyoguswa na tukio lililomkuta mbunge mwenzao huku wakisema wanaamisi vyombo vya ulinzi na usalama vitabaini chanzo cha matukio hayo.

Katika hatua nyingine bunge limepitisha bila kijadiliwa azimio la bunge la kuridhia itifaki ya tano ya mwaka 1994,itifaki ya nyongeza ya sita ya mwaka 1999 itifaki ya saba ya mwaka 2004,nyongeza ya nane ya mwaka 2008 na nyongeza ya tisa ya mwaka 2016 ya katiba ya umoja wa posta duniani.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>