Published On: Fri, Sep 8th, 2017

SIMIYU KULINDA VYANZO MAJI .

Share This
Tags

 

Viongozi wa vijiji,vitongoji  na kata  wilayani MASWA mkoani SIMIYU wametakiwa kuwaelimisha  wananchi kuvilinda vyanzo vya maji kwa kutumia sheria ndogo ili kuwabana wanaoviharibu  kwa  shughuli za kibinadamu  kwa kuacha mita 60.

Agizo hio limetolewa na mbunge wa jimbo la MASWA Magharibi MASHIMBA NDAKI wakati wa mkutano wake wa kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa vijiij vya MWABOMBA na MWANUNDI.

MASHIMBA  amesema pamoja uwepo wa mabadiliko ya  tabia nchi yaliyopelekea  vyanzo vingi vya maji kukauka na kusababisha kukosekana kwa  mvua  ,jitihada za dhati zinatakiwa za kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kulinda vyanzo hivyo.Nao wananchi wa vijiji hivyo wameelezea adha kubwa wanazozipata wakati wakitafuta maji huku wakilalamika kupoteza muda mwingi ambao wangeweza kufanya shughuli zingine za kimaendeleo.

Akijibu kero hizo mbunge wa jimbo la MASWA magharibi MASHIMBA NDAKI amesema katika kutatua changamoto ya maji  inayowakabili wananchi wake  tayari ameshafanya mazungumzo na  makubaliano   na wizara ya juu ya kuyatoa maji ya ZIWA VICTORIA  kutokea  wilaya ya  KAHAMA

tayari wameshapatiwa fedha kiasi cha shilingi milioni 20 kwa ajiri ya kufanya  upembuzi nyakinifu wa maeneo sahihi ya kupitisha mradi huo utakaowanufaisha wakazi wa jimbo hilo .

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>