Published On: Wed, Sep 13th, 2017

Serikali kurahisisha upatikanaji wa taulo za kike

Share This
Tags

Serikali imesema fedha za msaada zilizotolewa na benki ya dunia kwa ajili ya ukarabati wa vituo 100 vya upasuaji katika halmashauri mbalimbali nchini, zimeshapelekwa katika vituo hivyo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali la kuwa na huduma ya upasuaji katika zahanati zote nchini.

Pamoja na hatua hiyo pia serikali imeongeza muda kwa halmashauri kukarabati vyumba ya upasuaji katika vituo vyao vya afya ili kuokoa maisha ya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

Naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dk HAMIS KIGWANGALA ametoa taarifa hiyo wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum KHADIJA NASSIR ALI lililouliza kwa kiasi gani agizo la Mwandoya la serikali limetekelezwa.

Naibu waziri KIGWANGALA pia akawataka wabunge wote kusimamia ujenzi na ukarabati wa vyumba vya upasuaji kwenye vituo vya afya ambavyo vipo katika majimbo yao ili kurahisisha ufuatiliaji.

Katika hatua nyingine wizara ya afya maeneleo ya jamii jinsia wazee na watoto ipo katika majadiliano na wizara ya fedha  ili kuangalia namna ya kujumuisha taulo za kike katika vifaa tiba ili kupata msamaha wa kodi na kuongeza upatikanaji wake kwa bei nafuu.

Akijibu swali la mbunge wa viti maalum Stella Ikupa, Waziri wa afya UMMY MWALIMU amesema kuwa upatikanaji wa taulo hizo kwa sasa ni changamoto hivyo wizara hiyo inaangalia namna ya kurahisisha upatikanaji kwa kuondoa kodi katika bidhaa hiyo.

Ni Mkutano Wa Nane Kikao Cha Saba Ambapo Bunge Limepitisha Muswada Wa Sheria Ya Reli Tanzania ya Mwaka 2017.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>