Published On: Wed, Sep 13th, 2017

RC Arusha kusaidia ujenzi wa zahanati

Share This
Tags

Ukosefu wa maji na zahanati katika vijiji vilivyomo ndani ya  kata ya Musa, ni baadhi ya mambo yanayotajwa kama kikwazo cha maendeleo kwa wakazi wa kata hiyo hususani wanawake,ambao hutembea zaidi ya kilomita kumi  kutafuta huduma hiyo muhimu.

Baadhi ya wananchi wa kata hiyo wamebainisha hali hiyo katika ziara ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo yenye lengo la kutatua kero zinazowakabili wananchi wa wilaya ya Arumeru.

Baada ya kusikiliza kero na majibu ya wataalam, mkuu wa mkoa wa Arusha akawahakikishia wananchi wa kata ya Musa, kuwa iwapo wataonesha nia kwa kutoa eneo la ujenzi wa zahanati na kuanza ujenzi anatafanikisha ujenzi wa zahanati  hiyo.

Ni siku ya tatu ya ziara ya mkuu wa mkoa  wa Arusha Mrisho Gambo akiendelea kutatua kero za wananchi wake, ambapo amekuwa akitoa vifaa vya ujenzi kama cement,mabati na fedha taslimu katika miradi mbalimbali.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>