Published On: Mon, Sep 11th, 2017

RAIS MAGUFULI AMWAPISHA JAJI MKUU LEO

Share This
Tags

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. JOHN POMBE Magufuli amemuapisha PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA anakuwa Jaji Mkuu wa nane baada ya uhuru na hafla ya kuapishwa kwake imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN, Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JOB YUSTINO NDUGAI.

Akizungumza baada ya kumuapisha, Rais MAGUFULI amempongeza Jaji Mkuu na Majaji wengine wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani kwa kazi kubwa wanayofanya, na amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa mhimili huo wa dola ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto mbalimbali kulingana na uwezo wa kibajeti.

Aidha Rais MAGUFULI ametoa wito kwa Jaji Mkuu, Majaji na Mahakimu wote wa mahakama nchini kuongeza kasi ya kufanyia kazi changamoto mbalimbali za mahakama ikiwemo ucheleweshaji wa kesi, na kuongeza msukumo katika kushughulikia tatizo la rushwa.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>