Published On: Tue, Sep 12th, 2017

Rais Magufuli amjulia hali Meja Jen. Mstaafu Vincent Mritaba hospitali ya Jeshi Lugalo Dar es Salaam

Share This
Tags

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo ametembelea hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo,Jijini Dar es Salaam na kumjulia hali Meja Jen.Mstaafu Vincent Mritaba   aliyelazwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wakati akiingia nyumbani kwake Ununio, Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Meja Jen.Mstaafu Mritaba alishambuliwa kwa risasi jana tarehe 11 Septemba, 2017 majira ya mchana na kisha kukimbizwa katika hospitali ya Jeshi Lugalo kwa matibabu.

Mkuu wa kituo cha tiba cha hospitali hiyo na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Brigedia Jenerali Paul Massawe amemueleza Rais Magufuli kuwa Meja Jen.Mstaafu Vincent Mritaba anaendelea vizuri baada ya madaktari kufanikiwa kutoa risasi alizopigwa mkononi, kiunoni na tumboni.

Meja Jen.Mstaafu Mritaba amemshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa kumjulia hali na kumuombea dua iliapone haraka.

Rais Magufuli aliyeongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jen.Venance Mabeyo pia ametembea wodi ya majeruhi na kuwajulia hali wagonjwa wanaotibiwa katika wodi hiyo na baadaye akawasalimu wananchi waliofika hospitali hapo kwa ajili ya kupata matibabu.

Dkt. Magufuli amewapongeza Madaktari wa hospitali ya jeshi Lugalo kwa huduma za matibabu wanazotoa kwa askari na wananchi wengine na amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>