Published On: Thu, Sep 14th, 2017

PACHA WALIOUNGANA WAJIUNGA CHUO KIKUU TANZANIA

Share This
Tags

Pacha walioungana Maria na Consalata, nchini wameanza masomo yao katika chuo kikuu ili kujifunza kuwa walimu.

Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen, Pacha hao waliwashukuru walimu wao wapya kwa mapokezi mema waliopata mbali na mazingira mazuri ya kusoma waliopata yalioandaliwa na chuo kikuu cha Ruaha Catholic University.

Waliwasili katika chuo hicho mbele ya wanafunzi wengine ili kuweza kujiandaa na mazingira yaliyopo.

Walianza masomo yao ya Kompyuta Jumatano na kuwashukuru Wamishenari wa Consalata kwa kufikia kiwango hicho katika maisha yao.Wamishenari hao waliwalea na kuwashawishi kuendelea na masomo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>