Published On: Mon, Sep 11th, 2017
World | Post by jerome

OPERESHENI YA KIUSALAMA DHIDI YA WAISLAMU WA ROHINGYA NCHINI MYANMAR YAFANANISHWA NA MAUAJI YA KIKABILA

Share This
Tags

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ZEID RAAD AL HUSSEIN amesema Operesheni ya kiusalama inayowalenga waislamu wa Rohingya nchini Myanmar ni mfano wa mauaji ya kikabila.

HUSSEIN ameitaka Mynamar kusitisha operesheni mbaya ya kijeshi katika jimbo la Rakhine.

Zaidi ya watu 300,000 waisilamu wa Rohingya, wamekimbia kwenda Bangladesh tangu ghasia zianze mwezi uliopita.

Jeshi linasema kuwa linajibu mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa Rohingya na kukana kuwalenga raia.

Ghasia hizo zilianza tarehe 25 mwezi Agosti wakati wapiganaji wa Rohingya walishambulia vituo vya polisi kaskazini mwa Rakhine na kuwaua maafisa 12 wa ulinzi.

Rohingya ambao wameikimbia Myanmar tangu wakati huo, wanasema kuwa wanajeshi walijibu vikali kwa kuchoma vijiji na kuwashambulia raia kwa minajili ya kuwafukuza.

Rohinga ambayo ni jamii ndogo ya waislamu wasio na utaifa wamekumbwa na mauaji kwa muda mrefu nchini Myanmar ambayo inasema kuwa wao ni wahamiaji haramu.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>