Published On: Mon, Sep 11th, 2017

MTOTO ALIENUSURIKA KUUAWA NA SIMBA: AFYA YANGU INAENDELEA KUIMARIKA

Share This
Tags

Hatimaye Afya ya Mtoto TABANGILA MADIRISHA imeimarika baada ya kulazwa katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Kufuatia kujeruhiwa na Simba aliyevamia katika kijiji cha Isinde Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi.

Akizungumza nyumbani kwao mtoto huyo mwenye umri wa miaka 13 amesema afya yake inaendelea kuimarika licha ya kuwa na maumivu kiasi.

Baba Mzazi wa Mtoto huyo MADIRISHA LUBHINZA ameitupia lawama serikali kwa kushindwa kufika hata kumjulia hali wala kutoa msaada wa aina yoyote.

Simba huyo alijeruhi mtoto mmoja, aliua mifugo aina ya ng’ombe zaidi ya 10 na mbuzi saba ambapo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Nsimbo MAILWA PANGANI ameshabainisha mikakati ya kumdhibiti samba huyo.

Afisa wanyama Pori  Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo  SHABANI MATWILI amewataka wananchi kutokuweka Makazi yao Karibu ama ndani ya Hifadhi za Wanyama ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza kwao.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>