Published On: Wed, Sep 13th, 2017
World | Post by jerome

Merkel apata upinzani mashariki mwa Ujerumani

Share This
Tags

Ikiwa ni chini ya wiki mbili tu hadi tarehe ya uchaguzi mkuu wa Ujerumani unaofanyika tarehe 24 Septemba, Kansela Angela Merkel anaonekana kupata upinzani mkali kwenye upande anaotokea mwenyewe – mashariki.

Njiani kuelekea K├Âthen tukitoka mji mkuu Berlin kupitia Bitterfeld, ilikuwa dhahiri kwamba tofauti na maeneo ya magharibi mwa Ujerumani, mabango yanayomuonesha Kansela Angela Merkel anayepigiwa upatu kushinda uchaguzi huu, ni nadra sana kuyaona.

Hapa mashariki mwa Ujerumani, ambako ndiko anakotoka kansela huyo, umaarufu wake ulishuka sana mnamo miaka miwili iliyopita, kutokana na sera yake ya kufungua milango kwa wakimbizi.

Pigo kubwa alilolipata lilikuwa katika mji wa Bitterfeld katika eneo hili, ambako chama cha Christian Democratic (CDU) kilipigwa kikumbo na chama chenye misimamo mikali ya kizalendo kijiitacho Mbadala kwa Ujerumani (AfD) katika uchaguzi wa bunge mapema mwaka huu.

Lakini sasa, kulingana na maoni ya watu ambao tumewakuta katika hadhara hii ya chama cha Die Linke, ambayo ilihutubiwa na kiongozi wake maarufu, Gregor Gysi, ni kwamba chama cha AfD mara hii hakitafua dafu.

Gysi mwenyewe, ambaye ni mbunge katika bunge la shirikisho, alisema katika mkutano huo, kwamba inachopaswa kukifanya Ujerumani katika kupambana na tatizo la wakimbizi, ni kupinga mizozo inayosababisha watu kukimbia.

“Mtazamo wangu ni kwamba ni bora kuzuia mizozo inayosababisha vita. Kwa mfano, katika vita vinavyoongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen, wakimbizi watakuja hapa Ujerumani. Ujerumani ni miongoni mwa wasambazaji wa silaha zinazotumika katika vita hivyo. Je, baada ya mzozo wa wakimbizi wa mwaka 2015, isingekuwa uamuzi mzuri kusitisha mauzo ya silaha kwa nchi hizo?”

Gysi ambaye anafahamika kwa misiamamo yake ya kupinga vikwazo dhidi ya Urusi, alisema serikali ijayo ya Ujerumani inapaswa kujikita katika kuepusha mizozo duniani badala ya kuhusika kuisababisha.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>