Published On: Tue, Sep 12th, 2017
World | Post by jerome

Marekani yalaani machafuko dhidi ya Warohingya

Share This
Tags

Ikulu ya Marekani imelaani ongezeko la machafuko nchini Myanmar ambalo limewalazimu waislamu laki tatu wa jamii ya Rohingya kukimbilia nchi jirani ya Bangladesh.

Msemaji wa ikulu Sarah Huckabee amesema Marekani ina wasiwasi mkubwa kuhusu mzozo unaoendelea Myanmar na amelaani mashambulizi dhidi ya maeneo ya jeshi la nchi hiyo yaliyofanywa na wanamgambo wa Rohingya tarehe 25 mwezi uliopita na ukandamizaji wa jeshi uliofuatia.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litakutana kesho kujadili machafuko katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar. Wakati haya yakiarifiwa raia kadhaa wa Israel wenye asili ya kiarabu wameandamana nje ya ubalozi wa Myanmar mjini Tel Aviv kupinga jinsi Waislamu Warongya wanavyotendewa na utawala. Maandamano hayo ya jana yaliandaliwa na vuguvugu la kiislamu nchini Israel.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>