Published On: Mon, Sep 11th, 2017

MALARIA, UKIMWI , MFUMO WA UPUMUAJI, MOYO NA UPUNGUFU WA DAMU VYATAJWA KUONGOZA KUSABABISHA VIFO KWA BINADAMU.

Share This
Tags

Utafiti uliofanywa na taasisi ya taifa ya magonjwa ya binadamu NIMR tokea mwaka 2006  hadi mwaka 2015  katika hospitali 39 nchini  umebaini magonjwa ya malaria ,Ukimwi , mfumo wa upumuaji, magonjwa ya moyo pamoja na upungufu wa damu yanaongoza kusababisha vifo 247,976 kwa binadamu.

Vifo vingi vimetajwa kutokea katika mikoa ya Dar es Salaam , Morogoro na Mwanza .

Madhumuni makubwa ya tafiti hizo ni kuainisha matukio ya vifo katika hospitali nchini ili kutambua ongezeko la maradhi yanayoathiri jamii pamoja na kuchunguza uwepo, upatikanaji pamoja na ubora wa takwimu za vifo hospitalini.

LEONARD MBOERA ni mtafiti mkuu kiongozi  kutoka NIMR aliyebainisha kuhusu tafuti hizo za vifo walizozifanya.

Utafiti huo umehusisha hospitali 39 zikiwemo hospitali za Rufaa za Kanda, hospitali za mikoa, hospitali za wilaya pamoja na hospitali maalumu kote nchini.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>