Published On: Sat, Sep 30th, 2017

Kufanya kazi ndogo ndogo ya nyumbani kunaweza kuboresha maisha ya wazee.

Share This
Tags

Kubeba bidhaa waliyonunua, kufanya ukulima kidogo kwenye bustani na kusafisha nyumba kunaweza kuwasaidia watu wazee kuwa na maisha marefu yenye afya, kulingana na wataalamu wa afya.

Madaktari wanasema kuwa mamilioni ya watu wazee huanguka kila mara kwa sababu hawafanyi mazoezi.

Robo ya watu walio na umri wa zaidi ya miaka 65 hawafanyi mazoezi yoyote ya kuwapa nguvu, kulingana na madaktari ambao wanaonya kuwa kuongezeka kwa nafasi za kunua bidha mitandaoni kunamaanisha kuwa watu hawaendi madukani na kubeba bidhaa kutoka huko hadi nyumbani kwao.

Madaktari wanasema kuwa watu wengi hawafahamu umuhimu wa kufanya mazoezi ya kuwapa nguvu wanapoendelea kuongeza miaka.

Ni vyema kwa watu kufanya mazoezi ya kuwapa nguvu angalau mara mbili kwa wiki, kama kubeba mizigo mizito. Lakini utafiti uliohusisha zaidi ya watu wakongwe elfu mbili nchini Uingereza ulionyesha kuwa wengi wao hawafanyi mazoezi kamwe.

Mmoja kati ya watu watano alisema hawajui kufanya mazoezi na wengine walisema hawataki tu kuyafanya.

Ajali za kuanguka miongoni mwa watu wazee huchangia asilimia kubwa ya majeraha inayohusisha kuvunjika kwa mifupa ya sehemu ya kiuno, na hugharimu takriban dola bilioni moja kutibu kila mwaka.

Profesa Karen Middleton, ni afisa mkuu mtendaji wa CSP, na anasema tunakuwa dhaifu tunapokuwa wazee.

“Utafiti unaonyesha kuwa kufanya mazoezi ya kutupa nguvu kuna faida nyingi na ni muhimu watu kuzingatia haya.”

Anasema inaweza kuwa kupalilia shambani au kusimama mara 10 kutoka kwenye kiti.

“Siku hizi tunabeba mifuko chache sana tukitoka dukani na mara nyingi tunanunua bidhaa mitandaaoni.”

Profesa Middleton anasema kubeba mifuko ya chakula na bidhaa nyingine kutoka sokoni kunachangia mazooezi kwenye misuli.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>