Published On: Wed, Sep 13th, 2017
World | Post by jerome

Korea Kaskazini kujiimarisha baada ya vikwazo

Share This
Tags

Korea Kaskazini leo imeapa kuuharakisha mpango wake wa silaha za nyuklia kama hatua ya kujibu vikwazo ilivyowekewa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa baada ya jaribio lake la sita na kubwa kabisa la silaha za nyuklia.

Wizara ya mambo ya nchi za kigeni ya Korea Kaskazini imesema katika taarifa kwamba taifa hilo litaongeza maradufu juhudi za kujiimarisha ili kuulinda uhuru na haki yake.

Vikwazo vipya vilivyoandaliwa na Marekani vilipitishwa siku ya Jumatatu na vinajumuisha marufuku ya kuuza nguo katika nchi za nje na kudhibiti usafirishaji wa bidhaa za mafuta kuuadhibu utawala wa Pyongyang kwa jaribio hilo.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema hatua kali zaidi zinahitaji kuchukuliwa dhidi ya Korea Kaskazini baada ya vikwazo vipya vya Umoja wa Mataifa.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>