Published On: Tue, Sep 26th, 2017
Sports | Post by jerome

Kocha wa timu ya jang’ombe Zanzibar atamba dhidi ya zimamoto kwenye michuano ya ligi kuu

Share This
Tags

Kocha wa timu ya Taifa Jang’ombe Salehe Maisara amesema timu yake haina shaka na mchezo wao wa kwanza wa oktoba 5 watakaocheza na timu ya Zimamoto kwenye mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar msimu huu.

Maisara ametoa kauli hiyo kwenye mechi ya kirafiki na timu ya vijana Majengo ya jijini Tanga ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao dhidi ya mpambano wa ligi kuu visiwani humo.

Kocha huyo ametamba kukabiliana na Zima moto akisema wamejiandaa kuondoka na pointi tatu kwenye mchezo huo.

Licha ya kutoka droo ya goli moja kwa moja na timu hiyo imesema iko timanu kwa ajili ya mpambano huo  utakaoanza kutimua vumbi oktoba 3 mwaka huu huko visiwani Zanzibar.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>